Mambo 10 Usiyofahamu Kuhusu Money Heist (La Casa De Papel)

 • #MoneyHeist #LaCasaDePapel
  Kwa wale mashabiki wa Televisheni watajua, hakuna raha kama kusubiri episodes za Newzfid, kumradhi episodes za series. Tena kwa kipindi hiki mambo ni murua kabisa pale utaclick mara chache tu mpaka kuikuta series mpya ya La Casa de Papel maarufu kama Money Heist katika mtandao wa Netflix. Series hii inaelezea kisa cha kusisimua cha wezi wakiongozwa na profesa kuiba pesa katika taasisi ya kuchapisha fedha Royal Mint of Spain.
  1. Mfululizo huo ulitungwa na mwandishi Álex Pina na director Jesús Colmenar wakati wa miaka yao ya kushirikiana tangu 2008.
  2. Swali ambalo huulizwa zaidi katika mtandao wa Google ni "Je, Money Heist inahusu visa vya stori ya kweli".Jibu halisia ni kwamba, hapana lakini kwa namna fulani matukio ya series yanafanana na matukio halisi yaliyowahi kutokea na kuitikisa dunia.
  3. Kama tulivyojifunza katika msimu wa kwanza, majambazi hao hujificha na mask ambazo hufanania sura ya mchoraji wa Uhispania Salvador Dalí, ambaye kwa kawaida alikuwa na masharubu yaliyozidi.
  4. Wimbo wa Kiitaliano wa kupingana na fascism ya Benito musolini uitwao "Bella ciao" ulichezwa kwa mara ya kwanza pale Professor na Berlin wakiwa katika maandalizi ya kuiba pesa kutoka Royal Mint: Neno Bella Ciao linamaanisha kwaheri mrembo.
  5.La Casa De Papel ilizinduliwa katika channel ya Antena 3 mnamo tarehe 2 Mei 2017, na season ya kwanza ikiwa katika sehemu tisa.
  6. Mfululizo huo unaonyeshwa kupitia machoni mwa Tokio, msichana kichwa-moto, mtata ambaye alijikuta akimpenda sana Rio wakati wa 'mishe' yao ya wizi.
  7. Álvaro Morte ambae ameigiza kama Sergio "El Profesor" ni nani haswa? ni swali ambalo mashabiki wa Money Heist wanauliza. Basi jua kuwa,Sergio ndie aliyeweka sauti ya Gwangi katika toleo la kihispania la animationa ya Small Foot uhusika ambao ulishikwa na LeBron James katika toleo la asili.
  8. Shah Rukh khan, kipenzi cha mashabiki wa bollywood anaweza kuwa professor katika filamu ya Money Heist? Mara ya mwisho ya Khan kuonekana kwenye filamu ya Zero ambayo ilionekana kufeli vibaya, khan hajatangaza filamu yoyote katika ripoti za miezi nane zilizopita hata hivyo palikuwa na uvumi kuwa Shah Rukh Khan ana mpango wa kurudia onyesho la Money Heist kuwa filamu ya Kihindi.
  9. Je wajua kuwa kundi lote la profesa walitakiwa wawe wagonjwa walio hatarini kupoteza maisha na sio Berlin peke ake? Pia,Ifahamike kuwa jengo la Royal Mint ya Uhispania sio la ukweli badala yake wakaruhusiwa kutumia Baraza la Utafiti la Kitaifa la Uhispania huko Madrid.
  10. Karibu timu yote ya Money Heist walichagua miji mikuu ya kitaifa kama majina yao ya utani: Berlin (Ujerumani), Helsinki (Finland), Moscow (Russia), Nairobi (Kenya), Oslo (Norway), na Tokyo (Japan).

  Category : Séries streaming

  #mambo#10#usiyofahamu#kuhusu#money#heist#la#casa#de#papel


Description du streaming: >>> Cliquez-ici pour Télécharger <<<

Regarder en Streaming
  0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up